Jan 9, 2026 Vijana Njombe

Ujuzi wa Ajira na Ujasiriamali kwa Vijana

Maelezo ya Mafunzo
Vijana Njombe kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaandaa mafunzo maalum yenye lengo la kuwajengea vijana ujuzi wa kupata ajira na kuanzisha miradi binafsi. Mafunzo haya yanalenga kuwawezesha vijana kujitambua, kuboresha wasifu (CV), na kutumia fursa zilizopo katika soko la ajira na ujasiriamali.

Mada Zitakazofundishwa

  • Jinsi ya kuandaa CV na barua ya maombi yenye mvuto

  • Mbinu za kutafuta kazi na fursa mtandaoni

  • Msingi wa ujasiriamali na kuanzisha biashara ndogo

  • Usimamizi wa fedha kwa vijana

  • Fursa za mikopo na ruzuku kwa vijana

Faida kwa Washiriki

  • Kupata cheti cha ushiriki

  • Ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wakufunzi

  • Mtandao wa mahusiano (networking) na waajiri na wajasiriamali

  • Taarifa za fursa za ajira na mafunzo yanayoendelea

📝 Jinsi ya Kushiriki
Jisajili kupitia tovuti ya Vijana Njombe au wasiliana nasi kwa simu/WhatsApp kwa maelezo zaidi.

👉 Usikose nafasi hii ya kujijengea kesho bora!

Shiriki Chapisho Hili

Chapisho Linalohusiana