TANGAZO LA FURSA YA UFADHILI WA MASOMO NCHINI UTURUKI
Serikali ya Jamhuri ya Uturuki, kupitia mpango wa Türkiye Bursları, inatangaza rasmi fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kimataifa kwa mwaka wa masomo __________.Scholarship hii inalenga wanafunzi wenye sifa stahiki wanaotaka kusoma katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Uturuki katika ngazi zifuatazo: Shahada ya Kwanza (Bachelor’s Degree) Uzamili (Master’s Degree) Uzamivu (PhD) Faida za Scholarship hii ni pamoja na: Ada ya masomo kulipiwa kikamilifu Posho ya kila mwezi Tiketi ya ndege (kwenda na kurudi) Malazi ya mwanafunzi Bima ya afya Mafunzo ya lugha ya Kituruki kwa mwaka mmoja Sifa za waombaji (kwa ufupi): Awe raia wa nchi nyingine isiyo Uturuki Awe na matokeo mazuri ya kitaaluma Awe ndani ya umri unaokubalika kwa ngazi anayoiomba Awe hajawahi kusoma au kuishi Uturuki kwa muda mrefu Namna ya kuomba: Maombi hufanyika mtandaoni bila malipo kupitia tovuti rasmi ya Türkiye Bursları:
